NEWS

Thursday 31 December 2020

Waitara afunga dampo mjini Tarime

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara (kushoto), akitoka kukagua jalala katika mtaa wa Starehe mjini Tarime, leo Desemba 31, 2020.

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara ameagiza kufungwa kwa dampo la takataka lililopo mtaa wa Starehe mjini Tarime mkoani Mara.


Waitara ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kufunga dampo hilo leo Desemba 31, 2020 alipofanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika eneo hilo.
 
 
Ameonesha kutoridhishwa na uwepo wa dampo hilo katikati ya makazi ya watu akisema linahatarisha afya za binadamu ambapo wakati wa mvua limekuwa likitiririsha uchafu kwenda kwenye makazi ya wananchi.


Naibu Waziri huyo ameelekeza uongozi wa Halmashauri hiyo kutenga eneo maalumu la kutupa takataka kijijini Magena, nje kidogo ya Mji wa Tarime.

 
Baada ya hapo, Waitara amekwenda kukagua mazingira katika soko la mazao ya kilimo la Rebu ambako ametoa maelekezo ya kuboresha usafi wa mazingira, kabla ya kuendelea na ziara yake katika mji mdogo wa Sirari.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waitara (wa nne kushoto), akikagua mazingira katika soko la mazao ya kilimo la Rebu mjini Tarime, leo Desemba 31, 2020.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages