NEWS

Monday, 15 March 2021

Wiki ya Maji kuanza kesho Machi 16

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga.
 

MAADHIMISHO ya Wiki ya Maji nchini yataanza kesho Jumanne Machi 16 na kuhitimishwa Machi 22, 2021 - yakiwa na kaulimbiu inayosema “Thamani ya Maji kwa Uhai na Maendeleo.”

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amesema wiki hiyo itaadhimishwa kwa kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 281 yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania zaidi ya trilioni moja.

 

Mhandisi Sanga ameongeza kuwa shughuli hizo zitafanyika sambamba na upandaji wa miti kwenye maeneo ya vyanzo vya maji.

 

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Maji ameelekeza kwamba maadhimisho hayo hayatahusisha mikutano, warsha au makongamano.

 

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages