NEWS

Saturday 13 November 2021

Future conservationists: Wasichana wa Tarime wang’ara Serengeti Safari Marathon 2021, Naibu Waziri awakabidhi zawadi

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja na watoto wa kike walioibuka washindi wa mbio za kilomita 5 leo.

WATOTO wa kike, Mary Emmanuel (12) na Angel Mugini (11), ambao ni wanafunzi kutoka wilaya ya Tarime mkoani Mara, wameng’ara kwa kufanya vizuri katika mbio za Serengeti Safari Marathon 2021, zilizofanyika mapema leo Novemba 13 ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Angel na Mary wameshiriki mbio za kilometa tano, wakiwa ni miongoni mwa watoto wachache walioshiriki na kumaliza mbio hizo, huku wakionekana kuwa na nguvu na wachangamfu.

Watoto Angel (kushoto) na Mary wakifurahia mbio hizo

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amewatunuki wasichana hao kitita cha fedha taslimu kila mmoja, baada kutunukiwa medali na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess.


Meneja Mradi wa Shirika la Uhifadhi la Frankfurt Zoological Society (FZS) ofisi za Serengeti, Masegeri Rurai (katikati) katika picha ya pamoja na watoto Angel (kushoto) na Mary walioibuka washindi wa mbio hizo.

Mbio hizo zilizopewa jina la “Be part of the Migration”, zimeshuhudia mamia ya washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages