VIFAA mbalimbali vya ujenzi ikiwemo saruji, mabati na nondo vyenye thamani ya shilingi milioni 54.4 vimenunuliwa ili kuunga mkono nguvu za wananchi na kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jimbo la Musoma Vijijini.
Kiasi hicho cha fedha kimetolewa na Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge Profesa Sospeter Muhongo.
“Tunashukuru kwa msaada huu wa vifaa vya ujenzi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini kwani utatuepusha na michango. Wananchi wanajitolea kwa kiasi kikubwa, kwa hiyo utasaidia pale walipofikia. Tunampongeza sana Mbunge wetu, Profesa Muhongo kwa hili,” amesema Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyasaungu.
#MaraOnlineNews-Updates
No comments:
Post a Comment