NEWS

Friday, 19 July 2024

Mwanahabari kumlipa fidia Waziri Mkuu wa Italia baada ya kufanya mzaha juu ya kimo chake


Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, anaripotiwa katika vyombo vya habari vya Italia kuwa na urefu wa 1.63m (5ft 3in).

Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, anaripotiwa katika vyombo vya habari vya Italia kuwa na urefu wa 1.63m (5ft 3in).

Mwanahabari wa Italia ameagizwa kumlipa Waziri Mkuu Giorgia Meloni fidia ya €5,000 (£4,210) kutokana na machapisho ya mitandao ya kijamii yanayodhihaki urefu wake. 


Jaji aliamua kwamba jumbe mbili za Giulia Cortese katika mtandao wa kijamii wa X ambaye pia alipewa faini atakayolipa baadaye ya €1,200, zilikuwa za kumchafulia jina Waziri mkuu na zilidhamiria ‘kumuaibisha’ kwa sababu ya mwili wake. 


Ilifuatia mazungumzo ambayo Bi Cortese alimtaja Bi Meloni kama "mwanamke mdogo" na kumwambia: "Siwezi hata kukuona." 


Akijibu uamuzi huo, Bi Cortese alisema serikali ya Italia ina "tatizo kubwa la uhuru wa kujieleza na upinzani wa waandishi wa habari". 

 

Wawili hao waligombana kwa mara ya kwanza mnamo Oktoba 2021, wakati chama cha Bibi Meloni cha Mrengo wa kulia cha Brothers of Italy kilikuwa bado katika upinzani, baada ya Bi Cortese kuchapisha picha ya dhihaka ya Bi Meloni kwenye X, ambayo zamani ilikuwa Twitter. 

 

Bi Meloni alionekana kwenye picha akiwa amesimama mbele ya rafu ya vitabu ambapo picha ya dikteta wa kifashisti Benito Mussolini ilikuwa imeongezwa kwa njia ya bandia.



Mwanahabari Bi Cortese

 

Katika chapisho la Facebook, Bi Meloni alisema picha hiyo ilikuwa ya "dhamira mbaya" na kwamba atachukua hatua za kisheria.


Baadaye siku hiyo hiyo, Bw Cortese alisema kuwa alikuwa ameifuta picha hiyo baada ya kugundua kuwa ilikuwa ya uwongo.


Baadaye alisema katika chapisho tofauti :"Hunitishi, Giorgia Meloni. Baada ya yote, una urefu wa 1.2m [3ft 9in] tu. Siwezi hata kukuona."


Urefu wa Bi Meloni unaripotiwa katika vyombo vya habari vya Italia kuwa 1.63m (5ft 3in).

CHANZO:BBC


Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages