CEO wa Mara Online, Mugini Jacob (kushoto) akikabidhi kompyuta na printa kwa uongozi wa Shule ya Awali na Msingi Odikwa jana.
----------------------------------------
Shule ya Msingi Odikwa iliypo wilaya ya Rorya, mpakani na wilaya ya Tarime mkoani Mara imeadhimisha Mahafali ya Pili ya Darasa la Saba, huku CEO wa Mara Online, Mugini Jacob akiipatia msaada wa kompyuta moja, printa moja na vigae boksi tano ili kuunga juhudi za shule hiyo katika kuinua taaluma kwa wanafunzi.
Wahitimu wa Darasa la Saba wakiimba wimbo wa kumsifu na kumuomba Mungu wakati wa mahafali yao shuleni hapo jana.
-------------------------------------
Nao wajumbe wa Bodi ya shule hiyo walitangaza kuipatia shule hiyo msaada wa 'photocopy machine' yenye thamani ya shilingi milioni tatu.
Katika hotuba yake, Mugini ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, alipongeza uongozi na walimu wa shule hiyo kwa juhudi kubwa wanazofanya kuwapa wanafunzi elimu bora na kuendelea kuboresha mazingira ya shule hiyo.
Pia aliwapongeza wazazi na walezi kwa kuendelea kuwatimizia watoto wao mahitaji ya kusoma katika shule hiyo ya kutwa na bweni ya mchepuo wa Kiingereza.
CEO Mugini akisoma hotuba yake katika mahafali hayo. Wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Manga, Steven Gibai, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Awali na Msingi Odikwa, Samson Hagai (mwenye miwani) na Mkurugenzi wa shule hiyo, Jacob Nguka Okola (wa nne kutoka kulia).
--------------------------------------
Aidha, CEO huyo wa Mara Online aliwapongeza wahitimu hao kwa kufikia hatua hiyo, na kuwatakia mafanikio mema katika mitihani na masomo yao ya mbeleni.
“Endeleeni kumwomba Mungu, kusoma kwa bidii, kuheshimu wazazi, walezi, walimu na watu wote katika jamii,” aliwahimiza wanafunzi hao huku akiwambia kuwa safari ya kutimiza ndoto zao kimaisha inaanzia shule ya msingi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shule ya Awali na Msingi Odikwa, Jacob Nguka Ogola aliwashukuru wageni wote walihudhuria mahafali hayo na kuahidi kuwa wanafunzi hao watapata ufaulu wa juu katika Mtihani wa Taifa wa Kuhitimu Darasa la Saba kwani wameendaliwa vizuri.
"Mnaleta watoto wenu hapa ili tuwape ufaulu wa 'A', na siyo vinginevyo," alisema Nguka ambaye kitaaluma ni mwalimu.
Watahaniwa wote wa darasa la saba katika shule hiyo ya Odikwa kwa mwaka jana walipata ufaulu wa daraja A na kuifanya kushika nafasi ya kwanza kiwilaya na kufanikiwa kupeleka wanafunzi wawili katika shule za vipaji maalumu.
"Tumefanikiwa pia kuwa wa kwanza kiwilaya kwa miaka minne mfululizo, yaani 2020 - 2023) katika matokeo ya mitihani ya darasa la nne NECTA," ilisema sehemu ya risala ya wahitimu hao kwa mgeni rasmi..
Mahafali hayo yalihudhuriwa pia na Diwani wa Kata jirani ya Manga, Steven Gibai (CCM), miongoni mwa wageni waalikwa wengine.
No comments:
Post a Comment