NEWS

Friday, 30 August 2024

Gazeti la Sauti ya Mara latajwa Mkutano Mkuu wa HAIPPA PLC, CEO wake atunukiwa cheti cha pongezi



Viongozi wa HAIPPA PLC katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wakati wa Mkutano Mkuu mjini Musoma, Mara jana.
-------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Musoma

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Gazeti la Sauti ya Mara, Mugini Jacob ni miongoni mwa wadau waliotunukiwa vyeti vya pongezi katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa HAIPPA PLC uliofanyika mjini Musoma, Mara jana Agosti 29, 2024.

Bodi na Menejimenti ya HAIPPA PLC imemtunuku CEO Mugini cheti maalum cha kumpongeza, kutambua na kuthamini mchango wake kwa kampuni hiyo - kupitia Gazeti la Sauti ya Mara.

“Tunatambua mchango wako unaotuwezesha kufanikisha malengo yetu ya kuijenga HAIPPA PLC kuwa kampuni kubwa ya uwekezaji Tanzania inayoboresha maisha ya watu wengi,” HAIPPA PLC imesema kwenye cheti hicho.

Mgeni rasmi katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Kanali Evans Mtambi ambaye amewakilishwa na Mhandisi Mwita Okayo, ametuma wito kwa watu kujitokeza kwa wingi kununua hisa katika HAIPPA PLC ili kujikwamua kiuchumi.

RC Mtambi ameipongeza kampuni hiyo ya umma na kuahidi kuwa ofisi yake itaendelea kuiunga mkono katika juhudi za ubunifu na mipango ya kuwezesha wananchi ili kuinua uchumi na kuondoa umaskini katika jamii.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa HAIPPA PLC, CPA Boniface Thomas Ndengo amesema kampuni hiyo ilianzishwa Oktoba 27, 2022 kwa ajili ya kujishughulisha na uwekezaji, masoko, mitaji na ubunifu ili kushiriki uwekezaji wa miradi mikubwa na ya kimkakati nchini.

“Tulianza na wawekezaji wanane walionunua hisa 3,400 zenye thamani ya shilingi 1,700,000. Kufikia Desemba 31, 2023 tulikuwa na wanahisa 127 wenye mtaji wa shilingi 233,335,000, na hadi Agosti 28, 2024 mtaji wao ulikuwa shilingi 273,440,000,” amesema CPA Ndengo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya HAIPPA PLC, Dkt Bonamax Mbasa amesema kampuni hiyo imekuwa suluhisho la ukandamizaji lililokuwa likiwakabili wakulima, wafugaji na wavuvi katika masoko ya bidhaa zao.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages