Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kwenye ukumbi wa halmashauri jana. Kushoto ni Makamu wake, Thobias Elias Ghati na kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Gimbana Ntavyo.
--------------------------------------------
-------------------------------------
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara limemchagua Diwani wa Kata ya Nyamisangura, Thobia Elias Ghati kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa awamu ya nne mfululizo.
Uchaguzi huo ulifanyika wakati wa kikao cha baraza hilo kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo jana Agosti 14, 2024.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Gimbana Ntavyo alimtangaza Thobias kuwa mshindi wa nafasi hiyo baada ya kupata kura zote 11 za ndio.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote alimpongeza Thobias kwa ushindi huo na kutumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha madiwani kuendelea kuwahimiza wananchi kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Baada ya kutangazwa mshindi, Thobias aliwashukuru madiwani akisema “Niwashukuru sana madiwani wenzangu kwa namna ambavyo mmenipa ushirikiano na kunichagua kwa mara ya nne kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime. Niahidi kuendelea kuwapa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kusimamia maslahi yetu sote.”
Wakati huo huo, baraza hilo la madiwani limemwagiza Afisa Afya wa Halmashauri hiyo, Erasto Mbunga kushughulikia uhamisho wa jalala lililopo kata ya Nyamisangura kwenda eneo lililotengwa katika kata ya Nkende.
No comments:
Post a Comment