NEWS

Thursday 15 August 2024

DC Kanali Surumbu ahamishiwa wilaya ya Mbarali, Meja Gowele achukua nafasi yake Tarime



Kanali Maulid Hassan Surumbu
-------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
-----------------------------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amemhamisha Mkuu wa Wilaya (DC) Kanali Maulid Hassan Surumbu kutoka wilaya ya Tarime mkoani Mara kwenda wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt Moses Kusiluka jana Agosti 14, 2024, Rais Samia pia amemhamisha Meja Edward Flowin Gowele kutoka wilaya ya Rufiji mkoani Pwani kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime.

Vile vile, Rais Samia amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi wengine mbalimbali, akiwemo Prof Palamagamba Kabudi aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, huku William Lukuvi akiteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu.

Pia, Rais Samia amemteua Balozi Dkt Pindi Chana kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii akitokea Wizara ya Katiba na Sheria, na anachukua nafasi ya Angellah Kairuki ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais.

Naye Jenista Mhagama ameteuliwa na Rais Samia kuwa Waziri wa Afya iliyokuwa ikiongozwa na Ummy Mwalimu. Kabla ya uteuzi huo Jenista alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).  
Read Also Section

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages