Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko (katikati waliokaa mbele) wakifuatilia jambo katika Kongamano la Tano la Ekaristi Takatifu la Kanisa Katoliki jijini Dar es Salaam jana.
---------------
Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
------------------------
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Doto Biteko amewaomba Watanzania kuishi kwa kuvumiliana, kuheshimiana na kupendana kama ilivyoagizwa katika vitabu vya Mungu.
Dkt Biteko aliyasema hayo jana katika kilele cha Kongamano la Tano la Ekaristi Takatifu la Kanisa Katoliki lililofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Nalo Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limelaani utekaji na mauaji ya watu nchini na kutaka viongozi na watendaji wa vyombo vya usalama kutimiza majukumu yao ipasavyo ili kulinda heshima ya taifa.
“Sisi maaskofu hatuamini kuwa matukio haya ya kihalifu yana nguvu kuliko vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, hivyo tunaviomba vyombo vyetu hivi vitimize majukumu yao ili kurudisha heshima ya taifa letu ya kuwa kisima cha udugu na amani,” alisema Makamu wa Rais wa TEC, Askofu Eusebius Alfred Nzigilwa.
Kaulimbiu ya kongamano hilo inasema “Udugu Huponya Ulimwengu, Sisi sote ni Ndugu.”

No comments:
Post a Comment