Sehemu ya kikosi cha Argentina
Brazil na Argentina zimeshindwa katika mechi zao za hivi karibuni za kufuzu kucheza mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2026.
Brazil walichapwa 1-0 ugenini Paraguay, ikiwa ni kichapo cha nne katika mechi zao tano zilizopita za kuwaniwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia.
Kipa wa Liverpool, Alisson, kiungo wa Newcastle, Bruno Guimaraes na mchezaji wa West Ham, Lucas Paqueta walianza kucheza katika mechi hiyo.
Wachezaji watatu wa Real Madrid, Rodrygo, Endrick na Vinicius Jr walianza kama washambuliaji upande wa Brazil.
Mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia, Argentina, walipoteza kwa mabao 2-1 wakiwa ugenini dhidi ya Colombia, huku kiungo wa zamani wa Real na Everton, James Rodriguez akifunga bao la ushindi kwa mkwaju wa penalti.
Lionel Messi, ambaye sasa anachezea Inter Miami, hakuchezea Argentina.
Kiungo wa kati wa Manchester United, Manuel Ugarte, ambaye alijiunga na klabu hiyo mwezi uliopita akitokea Paris St-Germain, alianza kwa Uruguay katika sare ya 0-0 ugenini dhidi ya Venezuela.
No comments:
Post a Comment