NEWS

Thursday, 12 September 2024

Trump, Harris jino kwa jino mdahalo wa urais Marekani



Kamala Harris na Donald Trump

Na Mwandishi Wetu


Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris wa Chama cha Democratic na rais wa zamani, Donald Trump ambaye ni mgombea wa Chama cha Republican, jana walichuana vikali katika mdahalo wa kuelekea uchaguzi wa rais Novemba mwaka huu.

Wagombea hao walionekana wakishutumiana kwa kila mmoja wao kusema uwongo katika masuala ya msingi.

Kwa mfano bayana kuhusu uchumi, Harris alijibu kwa kumshambulia Trump kwa kumshutumu kuhusu utawala alipokuwa Rais kabla ya kurithiwa na Rais wa sasa, Joe Biden.

“Donald Trump alituacha na tatizo baya la ukosefu wa ajira tangu kutokea mdororo wa uchumi nchini Marekani. Tulichofanya ni kusafisha uchafu wa Trump,” Harris alisema.

Akijibu mapigo, Trump alisema maprofesa wa uchumi wameuchukulia mpango wake wa uchumi kuwa “wa kipekee” na “mzuri zaidi.”

Kuhusu uhamiaji, Trump alitoa madai yasiyo na msingi kwamba wahamiaji wanakula wanyama wa majumbani katika eneo la Spingfield, Ohio.”

“Wanakula mbwa, wanakula wanyama wa watu majumbani,” alidai.

Hata hivyo, mwongozaji wa mdahalo huo, David Muir, alibainisha kuwa hakuna ushahidi wa dai hilo.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages