NEWS

Thursday, 12 September 2024

Wafanyabiashara mbaroni wakitorosha dhahabu ya mabilioni

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akionesha mzigo wa dhahabu iliokuwa inatoroshwa.
 ------------------
 
Na Mwadishi Wetu, Dar es Salaam

Wafanyabiashara watatu wametiwa mbaroni bandarini Dar es Salaam wakitaka kutorosha dhahabu yenye uzito wa kilo 15.78 zinazokadiriwa kuwa na thamani ya Tsh bilioni 3.4.

Waziri wa Madini, Anthony Mavude aliwambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwamba serikali itafuta leseni za watu hao iwapo watapatikana na hatia mahakamani.

Alisema watu hao watawekwa kwenye orodha ya kutoruhusiwa kumiliki leseni ya kufanya biashara yoyote katika mnyororo wa thamani ya madini nchini.

Mavunde alifafanua kuwa watuhumiwa wamesema dhahabu hiyo ilikuwa ikisafirishwa kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar.

Alisema uchunguzi na mahojiano dhidi ya watuhumiwa hao vinaendelea na punde vikikamilika watapelekwa mahakamani kukabiliana na mkono wa sheria.

Waziri huyo alikipongeza kikosi kazi kwa kuzuia utoroshaji madini kwa ushirikiano na vyombo vingine vya dola.

Aliwaonya wafanyabiashara kuepuka tabia ya utoroshaji madini kwani inarudisha nyuma juhudi za serikali katika kukuza uchumi wa taifa.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages