NEWS

Thursday 5 September 2024

Rebecca Cheptegei, mwanariadha wa Uganda, afariki dunia baada ya shambulio la kinyama

Rebecca Cheptegei enzi za uhai wake
                                                            ---------

Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei amefariki dunia siku chache baada ya kumwagiwa mafuta ya petroli na kuchomwa moto na mpenzi wake wa zamani, amesema afisa wa Uganda.

Mwanariadha huyo wa umri wa miaka 33 kutoka Uganda, aliyeshiriki mbio za marathon jijini Paris, alikuwa na majeraha makubwa ya moto baada ya shambulio la Jumapili, daktari aliyekuwa akimtibu amesema.

Mamlaka katika kaskazini-magharibi mwa Kenya, ambapo Cheptegei aliishi na kufanyia mazoezi, wamesema alishambuliwa baada ya kurudi nyumbani kutoka kanisani.

Ripoti iliyowasilishwa na msimamizi wa eneo hilo ilidai kuwa mwanariadha huyo na mpenzi wake wa zamani walikuwa wakigombania kipande cha ardhi. Polisi wanasema uchunguzi unaendelea.

Kuna hofu kuhusu ongezeko la visa vya vurugu dhidi ya wanariadha wanawake nchini Kenya, vingi vikiisha kwa vifo.

"Tuna huzuni kubwa kutangaza kifo cha mwanariadha wetu, Rebecca Cheptegei mapema asubuhi ya leo ambaye kwa bahati mbaya alikuwa mwathirika wa vurugu za nyumbani. Kama shirikisho, tunalaani vitendo vya aina hii na kuitaka haki itendeke. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi," shirikisho la riadha la Uganda liliandika katika chapisho kwenye mtandao wa X.

Familia haijathibitisha kifo chake lakini Dk. Owen Menach, mkuu wa Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi huko Eldoret, ambapo alikuwa amelazwa, aliambia vyombo vya habari vya mitaa kwamba mwanariadha huyo alifariki baada ya viungo vyake vyote kufeli.

Mpenzi wa zamani wa Cheptegei pia alilazwa hospitalini - lakini akiwa na majeraha madogo ya moto.

Akizungumza na waandishi wa habari, mapema wiki hii baba yake, Joseph Cheptegei, alisema kuwa alikuwa akiomba "kwa ajili ya haki kwa binti yake," akiongeza kwamba hajawahi kuona kitendo cha kikatili kama hicho maishani mwake.

Kifo chake kinakuja miaka miwili baada ya mauaji ya wanariadha wenzake wa Afrika Mashariki, Agnes Tirop na Damaris Mutua, ambapo wapenzi wao walitambuliwa kama watuhumiwa wakuu katika kesi hizo na mamlaka.

Mume wa Tirop kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya mauaji, ambayo anakanusha, huku utafutaji wa mpenzi wa Mutua ukiendelea.

CHANZO:BBC
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages