NEWS

Tuesday, 10 September 2024

Trump na Harris wachuana vikali katika mdahalo wa urais

Bw. Donald Trump na Bi.Harris Kamala
                                                               ----------------------

Kamala Harris na Donald Trump wakabiliana vikali katika mdahalo wa urais uliofanyika nchini Marekani.

Wagombea hao wawili wameonekana wakishutumiana kwa kila mmoja wao kusema uwongo katika masuala kadhaa ya msingi.

Kwa mfano, katika suala la uchumi, Makamu wa Rais Kamala Harris amejibu kwa kumshambulia Trump akielekeza lawama kwa utawala wake.

"Donald Trump alituacha na ukosefu mbaya zaidi wa ajira tangu kutokea kwa mdororo mkubwa wa kiuchumi nchini Marekani," amesema.

"Tulichofanya ni kusafisha uchafu wa Donald Trump," Harris ameongeza.

Trump alijibu, akisema maprofesa wa uchumi wameuchukulia mpango wake wa kiuchumi kuwa "wa kipekee", na "mzuri zaidi".

Katika suala la uhamiaji, Trump ametoa madai yasiyo na msingi kwamba wahamiaji wanakula wanyama katika eneo la Springfield, Ohio.

"Wanakula mbwa. Wanakula wanyama wa nyumbani wa watu wanaoishi huko," Trump alisema.

Hata hivyo, muongozaji wa mdahalo huo David Muir alibainisha kuwa meneja wa jiji huko Springfield amesema hakuna ushahidi wa dai hilo.
Chanzo:BBC
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages