
Waziri George Simbachawene akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi katika Hospitali ya Halmashauri ya Musoma Vijijini jana. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
---------------------------------------------
Wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini ambao kwa muda mrefu walikuwa wakisafiri kwenda mjini Musoma kutafuta huduma za afya, sasa wameondokana na adha hiyo baada ya kujengewa hospitali ya kisasa katika kitongoji cha Kwikonero kijijini Suguti.
Jiwe la msingi la hospitali hiyo iliyogharimu shilingi bilioni 3.53 liliwekwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene.
Waziri huyo yuko mkoani Mara kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

Hospitali ya Halmashauri ya Musoma Vijijini ni moja ya miradi mikubwa ya uwekezaji kwenye sekta za kijamii katika mkoa wa Mara, iliyobuniwa ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
Vifaa tiba katika hospitali hiyo vimegharimu shilingi bilioni 2.2, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.
Wananchi wa jimbo hilo wameishukuru serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kugharimia ujenzi wa miradi inayowanufaisha moja kwa moja na kubadili hali zao za maisha.
Mkoa wa Mara katika miaka ya hivi karibuni umetekeleza miradi mingi ya kijamii katika sekta za afya, elimu, maji na miundombinu ya barabara kwa ustawi wa maisha ya wananchi kiuchumi na kijamii.
UNAWEZA PIA KUSOMA:
>>Wanakijiji Serengeti 'wamwangukia' Waziri Simbachawene, aagiza wajengewe daraja
a class="read-also-item" href="https://www.maraonlinenews.com/2024/10/waziri-simbachawene-akagua-miradi-ya.html">
>>Waziri Simbachawene akagua miradi ya elimu, maji Tarime
>>Sagini aweka wazi dhamira yake ya mageuzi ya elimu Butiama
>>DC Tarime aonya utumikishaji watoto kwenye mashamba ya bangi, ukatili wa kijinsia
No comments:
Post a Comment