NEWS

Tuesday, 1 October 2024

DC Tarime aonya utumikishaji watoto kwenye mashamba ya bangi, ukatili wa kijinsia



Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele akihutubia mkutano wa hadhara kijijini Nkerege leo.
-------------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime, Meja Edward Gowele ametoa onyo kali dhidi ya watu wanaotumikisha watoto kwenye mashamba ya zao haramu la bangi.

"Nimekuta watoto wadogo wanaotakiwa kuwa shule wanalimishwa kwenye mashamba ya bangi. Ni marufuku kuanzia leo, wengine wa kike wanakaa na wavuta bangi kule, tukimkamata tutaanza na mzazi, kweli tutakufunga," amesisitiza.

DC Gowele ametoa maonyo hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nkerege kilichopo kata ya Kiore, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) leo Oktoba 1, 2024.

Pia, amewataka wananchi wilayani humo kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia, ukiwemo ukeketaji.
Kamishina wa sheria kutoka DCEA,Veronica Matikila akifafanua sheria dhidi ya dawa za kulevya aina ya bangi kwenye mkutano wa hadhara
 -------------------------------
Kiongozi huyo wa wilaya ameambatana na wataalamu wa sheria kutoka ofisi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) kwa ajili ya kwenda kuwapa wananchi ufahamu wa kisheria juu ya dawa kulevya hizo ikiwemo bangi na madhara yake kijamii na kiuchumi


Awali, DC Gowele ambaye pia ameambatana na Diwani wa Kata ya Kiore, Rhobi Samwel na wataalamu wa halmashauri hiyo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, afya na maji inayoendelea kutekezwa katani humo.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages