Wenyeviti wa vijiji wakionesha mifano ya hundi za malipo ya gawio la mrahaba la shilingi bilioni 2.1 lililotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Barrick Norh Mara, mbele ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima (wa pili kushoto waliokaa), wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kitaifa Nyamongo, wilayani Tarime leo.
--------------------------------------
Kampini ya Barrick kwa mara nyingine tena imevipatia vijiji vitano vilivyo jirani na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara gawio la mrabaha la shilingi bilioni 2.1, ikiwa ni malipo ya robo ya tatu ya mwaka 2024.
Vijiji hivyo na kiasi cha fedha kilichopokewa kikiwa kwenye mabano ni Genkuru (746,461,112), Nyangoto (581,176,695), Kerende (454,221,570), Nyamwaga (225,997,310) na Kewanja (98,350,773).
Vijiji hivyo ni ambavyo vilikuwa na haki ya kuchimba dhahabu kwenye shimo la Nyabigena (ambalo ni sehemu ya mgodi wa North Mara) kabla ya Kampuni ya Barrick kukabidhiwa kuendesha mgodi huo kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals kuanzia mwaka 2019.
Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Apolinary Lyambiko, malipo hayo ya shilingi bilioni 2.1 yanafanya gawio la mirabaha iliyotolewa na Barrick North Mara kwa vijiji hivyo kutokana na uzalishaji wa Aprili 2023 hadi Septemba 2024 kufikia shilingi bilioni 4.471.
Mifano ya hundi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.1 imekabidhiwa kwa viongozi wa vijiji hivyo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima leo Desemba 9, 2024 wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika kitaifa Nyamongo wilayani Tarime, Mara.![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj4o7JX9RWQtsRLqk7XfCFPeluM4q1ZzRJSzxHE2C1iIm_KJir4WH4Bn8XfPq_q-PDIRPrEAMtSvg_wzVV8qppRzgXwXoQlRIoWevbnIW50lvBDDnIKTkHsynzLilCmiWatxT0QksGnh8AzCi6j_e_YRhL-n5SVzE3JydwEPj3bGJtRJxN4ljfrzpERkX8/w640-h436-rw/7.JPG)
Waziri Gwajima ameipongeza Barrick North Mara akisema utoaji wa gawio la mirabaha hiyo unasaidia kuboresha huduma za jamii na kuchochea maendeleo ya kisekta katika vijiji hivyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara amewaelekeza viongozi wa vijiji vilivyopata fedha hizo za mrabaha kuhakikidha wanashirikisha wananchi kupitia mikutano halali katika kuibua na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati.
Nao wenyeviti wa vijiji vilivyopata mrabaha wameshukuru na kuupongeza mgodi wa North Mara kwa namna unavyoendelea kuimarisha mahusiano na jamii inayouzunguka.
"Mgodi umekuwa na mahusiano mazuri na wananchi, hasa kwa kushirikiana katika nyanja za kimichezo na kimaendeleo, pia umekuwa ukitimiza wajibu wa kisheria kama Serikali inavyoelekeza, tunaushukuru sana," amesema Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyangoto, Zakaria Machage.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Genkuru, Juma Elias ameushukuru mgodi huo na kuahidi kwenda kushirikiana na wananchi wake kupanga matumizi mazuri ya fedha walizopata kwa ajili ya miradi ya maendeleo. "Fedha tunayo, sasa hakuna sababu ya kuchelewesha miradi," amesema.
Majiko hayo yametolewa na mgodi huo kwa kushirikiana na Kampuni ya Taifa Gas katika kuunga mkono jitihada za serikali za kumtua mama kuni kichwani na kumuepushia adha ya matumizi ya nishati ya kupikia isiyo salama.
No comments:
Post a Comment