NEWS

Monday, 3 February 2025

Tarime Vijijini: Nyambari aipatia Sekondari ya Nyansincha msaada wa vitabu vyenye thamani ya milioni 2/-



Mwakilishi wa Nyambari Nyangwine, Sospeter Migera Paul (wa tatu kutoka kulia) akikabidhi msaada wa vitabu katika Shule ya Sekondari Nyansincha, Tarime Vijijini juzi.
----------------------------------

Na Mwandishi Wetu/ Mara Online News

Mfanyabiashara, mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini, Nyambari Nyangwine - kupitia taasisi yake ya Nyambari Nyangwine Foundation (NNF), ameipatia Shule ya Sekondari Nyansincha msaada wa vitabu vya kiada na ziada vyenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni mbili.

Shule ya Sekondari Nyansincha iliyopo kata ya Nyansincha katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), inamilikiwa na Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Jimbo la Mara.

Nyambari ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mwaka 2010-2015 kwa tiketi ya chama tawala – CCM, aliwakilishwa na Sospeter Migera Paul katika kukabidhi msaada huo wa vitabu katika shule hiyo juzi.

NNF imekuwa ikitoa misaada ya kijamii, husuan elimu katika maneo mbalimbali nchini, ambapo inatarajia kugawa vitabu vyenye thamani ya shilingi zaidi ya mlioni 200 katika shule zote za sekondari zilizopo katika halmashauri zote mbili za wilaya ya Tarime.

Wiki iliyopita, Nyambari aliwatua wazazi na walezi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mangucha iliyopo kata ya Nyanungu, Tarime Vijijini mzigo wa michango ya fedha za kudurufu na kuprinti karatasi za mitihani, baada ya kuipatia shule hiyo msaada wa photocopy machine na printer mpya.

“Tunamshukuru sana Mhesimiwa Nyambari Nyangwine kwa msaada huu muhimu, sisi wananchi wa kijiji cha Mangucha tunaendelea kutambua na kuthamini michango yake mbalimbali ya kimaendeleo tangu akiwa Mbunge wa Jimbo la Tarime,” alisema Gideon Ngicha Mnyoro, mkazi wa kijiji cha Mangucha na Katibu wa CCM Tawi la Mangucha.
Mwakilishi wa Nyambari Nyangwine, Sospeter Migera Paul (mwenye fulana ya bluu) akikabidhi msaada wa photocopy machine na printer mpya katika Shule ya Msingi Mangucha. (Picha zote na Mara Online News)
------------------------------------

Akikabidhi msaada wa vifaa hivyo, Migera alisema Nyambari Nyangwine ambaye alisoma katika Shule ya Msingi Mangucha hakuona sababu ya kusita kutoa msaada huo baada ya kuombwa na uongozi wa shule hiyo wakati wa mahafali ya darasa la saba mwaka jana.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages