
Na Christopher Gamaina
Tarime
-------------

DC Edward Gowele

Tarime
-------------
Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime, Meja Edward Gowele, amehamasisha waandishi wa habari kutangaza vivutio adimu vya utalii, yakiwemo makundi ya nyumbu yanayovuka Mto Mara eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti upande wa wilaya hiyo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Umoja wa Kuwezesha Waandishi wa Habari (REU) mjini Tarime, Ijumaa iliyopita, DC Gowele alisema eneo hilo ni ‘maajabu ya dunia’ na hazina ya kipekee ambayo haijatangazwa ipasavyo.

DC Edward Gowele
Kiongozi huyo alisema kivutio hicho kikitangazwa ipasavyo watalii wengi kutoka maeneo mbalimbali duniani watamiminika kwenda kushuhudia maelfu ya nyumbu wanaovuka Mto Mara kwenda nchi ya Kenya na Kurudi Tanzania kila mwaka.
“Maajabu ya dunia yako pale [Kogatende]. Tutumie kalamu zetu kutangaza mazuri hayo, ni kivutio kikubwa kwenye wilaya yetu. Lakini pia kuna wawekezaji wakubwa wako pale. Kwa hiyo, mzunguko mkubwa wa fedha uko katika wilaya yetu,” alisema.
DC Gowele aliongeza kuwa endapo eneo hilo litapewa kipaumbele katika kutangazwa, Tarime itakuwa kitovu kipya cha utalii nchini, kwani wageni wengi watavutiwa kufika, kulala na kushuhudia mbashara uhamaji mkubwa wa wanyamapori hao.

No comments:
Post a Comment