NEWS

Wednesday, 8 October 2025

Dkt. Samia kutikisa kampeni za kuomba kura Mara



Dkt. Samia Suluhu Hassan

Na Mwandishi Wetu
Mara
----------

Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Oktoba 9, 2025 anaanza kuhutubia mikutano ya kampeni mkoani Mara.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya CCM Mkoa wa Mara inaeleza kuwa Dkt. Samia atahutubia mikutano ya hadhara ya wananchi katika wilaya za Butiama, Bunda, Musoma na Serengeti.

Dkt. Samia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, ataelezea mafanikio ya Serikali yake ya Awamu ya Sita chini ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020–2025, dira na mikakati mipya ya kuimarisha maendeleo ya wananchi.


Katika kuonesha uzito wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi (pichani kulia), jana alikagua maandalizi ya maeneo yatakayotumika kwa ajili ya mapokezi na mikutano ya Dkt. Samia.

Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unapangwa kufanyika nchini Oktoba 29, 2025.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages