
Dafroza Jacob “Mama Frank” enzi za uhai
Na Mwandishi Wetu
Tarime
------------
Dafroza Jacob aliyegombea udiwani kata ya Sirari kupitia ACT Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 29, 2025, amefariki dunia, ikielezwa kwamba aliugua ghafla wakati akichukuliwa maelezo katika kituo cha Polisi.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya inasema Dafroza maarufu kwa jina la Mama Frank alipoteza maisha alipofikishwa hospitalini, baada ya kuanguka ghafla kituoni hapo jana Novemba 5, 2025 saa saba mchana.
“Wakati akiwa anapatiwa matibabu alifariki dunia. Uchunguzi utafanyika kwa kushirikisha wataalamu wa uchunguzi wa vifo ili kubaini chanzo cha kifo chake,” ilihitimisha taarifa hiyo ya Polisi bila kutaja tuhuma alizokuwa akikabiliwa nazo.
No comments:
Post a Comment