
Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
-------------
Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki mkoani Singira, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (CCM), ameteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kisha kuthibitishwa na Bunge kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amethibitishwa leo Alhamisi Novemba 13, 2025 Bungeni jijini Dodoma kwa kura 369 za ndio kati ya 371 zilizopigwa na wabunge, mbili zikiharibika.
Dkt. Nchemba amemrithi mtangulizi wake, Kassim Majaliwa, ambaye ametumikia nafasi hiyo kwa miaka 10.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, Dkt. Nchemba alikuwa Waziri wa Fedha, nafasi ambayo ikuchukuliwa na kumpata mtu mwingine kwenye uteuzi wa Baraza la Mawaziri lijazo.
Dkt. Nchemba wanakuwa Waziri Mkuu wa 12 tangu nchi ipate uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1961.
Waziri Mkuu mteule huyo anatarajiwa kuapishwa na Rais Samia katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino, Dodoma kesho Ijumaa, Novemba 14, 2025.
No comments:
Post a Comment