NEWS

Wednesday, 31 December 2025

Rais Samia aipongeza Taifa Stars kwa mafanikio ya kihistoria AFCON



Sehemu ya kikosi cha Taifa Stars

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Timu ya Taifa ya mpira wa miguu, Taifa Stars, kwa kuandika historia mpya baada ya kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa timu hiyo.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii usiku wa kuamkia leo Jumatano, Rais Samia alisema mafanikio hayo yametokana na maandalizi mazuri na juhudi kubwa za wachezaji, akiwapongeza kwa kuliletea taifa heshima na furaha kubwa, huku akiwatakia kila la kheri katika hatua inayofuata.


Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

“Ninaipongeza timu yetu ya Taifa ya mpira wa miguu, Taifa Stars kwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu.

“Heshima hii kubwa kwetu ni matokeo ya maandalizi mazuri na kujituma kwenu katika kila mchezo. Mmeandika historia kubwa kwa Taifa letu na mmeleta furaha kwa Watanzania wote. Hongereni sana.

“Ninawatakia kila la kheri katika michezo inayofuata,” Rais Samia aliandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages