
Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Pius Lutumo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Musoma
.......................
Polisi mkoani Mara wamewakamata watu 27 kwa madai ya kufanya vurugu na kukaidi amri halali ya kutofanya maandamano.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa wanachama wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA).
Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Pius Lutumo, alitibithisha kukamatwa kwa watu hao katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Musoma jana.
Kamanda Lutumo alisema kabla ya kukamatwa kwa watu hao Jeshi la Polisi lilitoa katazo mapema baada ya kubaini kuwepo dalili za "maneno ya uchochezi".
RPC huyo alikanusha madai ya watu hao kwamba walizuiwa kuingia kanisani.
Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara
No comments:
Post a Comment