NEWS

Monday, 9 March 2026

Makamu Mwenyekiti Tarime DC: Tunawashukuru sana Barrick kwa miradi ya CSR inayogusa jamii



Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Juster Magabe (kulia). Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko.

Na Mwandishi Wetu
Nyamongo
-----------------

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Barrick hivi sasa inatazamwa kama chachu ya mageuzi makubwa ya maendeleo yanayofanyika katika vijiji vilivyo jirani na mgodi wake wa dhahabu wa North Mara uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

“Tuawashukuru sana Barrick kwa miradi ya CSR inayogusa jamii. Barrick sasa imekuwa ni sehemu ya jamii,” Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Juster Magabe, alisema hivi karubuni katika hafla ya kukabidhi jengo la nyumba pacha ya walimu katika Shule ya Sekondari Nyamongo.

Nyumba hiyo imejengwa kutokana na fedha zilizotolewa na Mgodi wa Barrick North Mara kupitia mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Mgodi huo umetumia shilingi milioni 124.6 kupitia mpango wake wa CSR kujenga nyumba hiyo kuunga juhudi zinazofanywa na serikali kuboresha makazi ya walimu.

“Tunawashukuru sana Barrick na tunaomba muendelee hivyo hvyo,” alisema Juster ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyakonga.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, alipokea mradi huo na kueleza kuridhika na viwango vya utekelezaji wake.

“Nimefarijika, nimekagua na kuridhika na mradi huu wa nyumba za walimu, mradi upo kwa viwango vizuri,” Kanali Mtambi alisema.

Aliwapongeza wafanyakazi wa Barrick kwa kusimamia vizuri utetekelezaji wa mradi huo ambao utasaidia kuboresha makazi ya walimu.

“Nawapongeza Barrick kwa weledi uliotukuka, viwango kwenye mradi huu ni vya kimataifa, hongereni sana,” aliongeza Mkuu huyo wa mkoa kwenye sehemu yake hotuba yake katika hafla hiyo.

Viongozi wa kijamii kutoka maeneo yanayozunguka mgodi huo walisema uwepo wa mgodi huo umewaletea maendeleo makubwa.

“Uwepo wa mgodi kwa kweli umeleta faida nyingi kwetu. Mfano, tumejenga vituo vya afya, miundombinu ya elimu, maji na barabara,” alisema Diwani wa Kata ya Kemambo, Rashid Bogomba.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Mahusiano wa Barrick North Mara, Francis Uhadi, ujenzi wa nyumba hiyo ni miongoni mwa miradi mipya ya CSR 51 ambayo imekamilika kwa asilimia 100, huku utekelezaji wa miradi mingine 52 ukiwa unaendelea katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages