NEWS

Wednesday, 8 April 2026

Bei ya mafuta yashuka kufuatia kusitishwa kwa vita ya Marekani, Israel dhidi ya Iran




Na Mwandishi Wetu

Makubaliano ya Marekani na Iran ya kusitisha vita kwa muda wa wiki mbili yamekuwa faraja duniani kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta.

Leo Jumatano Aprili 8, 2026 bei ya pipa moja la mafuta imeshuka hadi kufikia chini ya dola za Kimarekani 100, kwa mujibu chanzo cha Oilprices.com.

Wakati wa vita ya Marekani, Israel dhidi ya Iran bei za mafuta zilipanda ghafla, hasa baada ya Iran kuzuia meli zinazosafirisha shehena ya bidhaa hiyo kupitia mlango wa bahari wa Hormuz.

Tanzania ni moja ya nchi zilizoathirika na hali ya kupanda kwa ghafla kwa bei ya mafuta kama ilivyotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Baadhi ya wafanyabiashara katika sekta ya usafirishaji wamejichukulia mamlaka ya kupandisha nauli bila kufuata utaratibu uliowekwa na mamlaka husika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages