NEWS

Monday, 27 April 2026

Mbunge wa Serengeti awasilisha Bungeni kilio cha wananchi wanaopata madhila ya tembo



Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Mary Daniel Surati, akizungumza Bungeni jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu
Dodoma
-----------------

Serikali imeanza kutumia Mfumo wa Kielektroniki (Problem Animal Information System (PAIS) kurahisisha ukusanyaji na uwasilishaji wa taarifa za matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu wanaohatarisha maisha na kuharibu mali nchini, ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara.

Hayo yalibainishwa Bungeni jijini Dodoma wiki iliyopita na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamad Hassan Chande, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Mary Daniel Surati, aliyetaka kufahamu mpango wa serikali wa kulipa vifuta jasho na machozi kwa wakati kwa wananchi walioathiriwa na wanyamapori katika jimbo hilo.

Naibu Waziri Chande alibainisha kuwa mfumo huo tayari umeanza kufanya kazi na umesaidia kuongeza kasi ya uchakataji na uhakiki wa taarifa zinazowasilishwa, kuwezesha malipo ya kifuta jasho na machozi kufanyika kwa wakati na kupunguza udanganyifu wa taarifa zinazowasilishwa.

Alisema serikali imekuwa ikilipa kifuta jasho na kifuta machozi kama mkono wa pole au faraja kwa wananchi wanaopata madhara kwa lengo la kuimarisha mtazamo chanya kwa wananchi juu ya shughuli za uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori nchini na kusisitiza kuwa malipo hayo yamekuwa yakifanyika kwa mujibu wa kanuni za kifuta Jasho za Mwaka 2011 na Marekebisho yake ya Mwaka 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages