NEWS

Saturday, 30 May 2026

Mawaziri wa Ulinzi Tanzania, Msumbiji wakutana Dar, wasaini makubaliano ya ushirikiano wenye tija



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Tanzania, Dkt. Rhimo Nyansaho (kulia) na Waziri wa Ulinzi Msumbiji, Cristóvão Chume, wakisaini makubaliano ya ushirikiano wenye tija kwa nchgi hizo.

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
--------------------

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Rhimo Nyansaho, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri va Msumbiji, Cristóvão Chume, katika zilipokuwa ofisi za Makao Makuu va Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Upanga, jijini Dar es Salaam.

Kikao kikiendelea

Kikao cha mawaziri hao kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda na maafisa waandamizi kutoka wizara hiyo na Wizara ya Ulinzi ya Msumbiji.

Lengo la ziara hiyo ya Waziri Chume wa Msumbiji hapa Tanzania ni kuimarisha na kuendeleza ushirikiano katika masuala va ulinzi na usalama baina ya nchi hizo.

Waziri Chume na Waziri Nyansaho pia wamepata fursa va kusaini makubaliano mbalimbali ya ushirikiano yatakayochangia kuleta manufaa kwa pande zote mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages