
Nyambari Nyangwine (aliyevaa kofia) na ujumbe wake wakiwa tayari kwa ziara ya kuelekea nchini Uturuki.
Dar es Salaam
--------------------
Mfanyabiashara Mtanzania, Nyambari Nyangwine ameanza ziara ya kiabishara ya siku saba nchini Uturuki.
“Leo naelekea Turkey (Uturuki) kwa ziara ya siku saba baada ya kupata mwaliko kutoka kampuni za Uturuki zinazojihusisha na masuala ya afya, ujenzi, kilimo na uchapaji wa vitabu,” Nyangiwine amewambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Mei 5, 2026, muda mfupi kabla ya kuondoka kuelekea Uturuki.
Akiwa nchini Uturuku, Nyangwine na ujumbe wake watazuru katika miji ya Instanbul, Ankara na Konya.

Nyangwine ambaye pia ni mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini, amekuwa akitanua uwekezaji ndani na nje ya Tanzania katika miaka ya hivi karibuni.
Mwezi uliipita ( Aprili), Nyambari pia alifanya ziara ya kibiashara ya siku 11 nchini China katika miji ya Shangai na Guangzhou.
Nyambari ambaye ni Mwenyekiti wa Nyambari Nyangwine Group of Companies Ltd (NNGCL), pia ameanzisha kampuni mpya ya Nyambari Nyangwine Building and Constrictions ambayo inatarajiiwa kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi kwa kutumia vifaa na tekonolijia ya kisasa.
Mfanyabiashara huyo pia ni mwanasiasa ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, mkoani Mara kupitia chama tawala - Chama Cha Mapinduzi (CCM).
No comments:
Post a Comment