
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemhamisha Katibu Mkuu Eliakim Chacha Maswi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kwenda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, leo Mei 2, 2026, imesema Rais Samia pia amemhamisha Katibu Mkuu Dkt. John Antony Jingu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwenda Wizara ya Katiba na Sheria.
Wakati huo huo, Rais Samia amemteua Dkt. Evaline Wilbard Munisi kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), ambapo anachukua nafasi ya Rahma Riyadh Kisuo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
No comments:
Post a Comment