
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi, akitoa maelekezo ya utatuzi wa mgogoro wa familia ya Ruhumbika na mgodi wa dhahabu unaoendeshwa na Kampuni ya Wakazi Mining Limited.
Musoma
---------------
Hatimaye familia ya Ruhumbika Machumu Kasanje, mkazi wa kijiji cha Chirorwe wilayani Musoma, imelipwa shilingi milioni 43, zikiwemo milioni 40 za fidia na milioni tatu za usumbufu ili kupisha mgodi wa dhahabu unaoendeshwa na Kampuni ya Wakazi Mining Limited.
Kampuni ya Wakazi Mining Limited kutekeleza maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi, aliyoyatoa katika mkutano wa hadhara kijijini hapo jana Julai 21, 2026.
Julai 4, 2026, familia hiyo ilitoa malalamiko kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Suguti katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, ikiomba kulipwa fidia ili kupisha mgodi huo na kuodokana na usumbufu unaotokana na kelele na kurushiwa mawe kwenye makazi yake.
Kufuatia malalamiko hayo, Waziri Mkuu Mwigulu alimwagiza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara kusikiliza kero ya familia hiyo na kutoa mrejesho katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa ajili ya kutatua mgogoro huo.
Akizungumza leo Julai 22, 2025 baada ya familia hiyo kulipwa fidia na kuhama katika eneo hilo, Kanali Mtambi amepongeza hatua hiyo kwa kuwa inamaliza mgogoro uliodumu kwa muda mrefu na kuyaondoa maisha ya familia hiyo katika hatari za kiusalama.
“Kulipwa kwa fidia hiyo kunatuwezesha kuufungua tena mgodi huo uendelee na shughuli zake za uchimbaji wa madini, ambapo watu zaidi ya 400 wamepata ajira na maisha yao yanategemea mgodi huo,” amesema.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana Julai 21, 2026, Kanali Mtambi alitoa saa 24 kwa kampuni hiyo kkuhakikisha inailipaa familia hiyo fidia ya ardhi sambamba na fedha za usumbufu na kodi ya nyumba ya miezi sita ili iweze kupisha shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo.
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Msongera Parela, amesema tayari familia hiyo imeshapokea malipo ya fidia na imeishukuru serikali kwa kufanikisha utatuzi wa mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu.
Ndugu Parela amesema baada ya kupokea fidia hiyo, tayari familia hiyo imeshahama katika eneo hilo na kwamba kampuni ya Wakazi Mining Limited sasa iko huru kuendelea na shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment