
Shehemu ya wachezaji wa Timu ya Soka ya Hispania wakishangilia ushindi wa Kombe la Dunia 2026
Hispania imetwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2026 baada ya kuicha Argentina bao 1-0 katika mechi ya fainali iliyochezwa usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa New Jersey nchini Marekani.
Mchezaji Ferran Torres alikuwa shujaa wa Hispania alipoupokea mpira wa kichwa kutoka kwa mchezaji aliyeingia akitokea benchi, Nico Williams na kumshinda mlinda lango wa Argentina, Emiliano Martinez, kwa shuti kali la karibu katika dakika ya 106.

Ferran Torres, mfungaji wa bao pekee lililoipatia Hispania ubingwa huo.
Rais Donald Trump wa Marekani aliwasili New Jersey kwa msafara wa helikopta kabla ya mchezo kuanza, huku Shakira, Madonna na Justin Bieber wakitumbuiza katika onesho la kwanza kabisa la mapumziko ya kipindi cha kwanza katika historia ya Kombe la Dunia, na kufanya mapumziko hayo yadumu kwa dakika 27.
Katika mchuano huo Hispania ilionekana kuwa bora zaidi, huku Lamine Yamal na Mikel Oyarzabal wakimlazimisha Emiliano Martinez kuokoa mipira muhimu katika kipindi cha kwanza.
Mchezo ulizidi kuwa mkali katika dakika za nyongeza za muda wa kawaida, ambapo Enzo Fernandez, ambaye tayari alikuwa ameonywa kwa kadi ya njano, alipata kadi ya pili ya njano kwa kumchezea vibaya beki wa Hispania Pau Cubarsi na hivyo kutolewa nje.
Argentina ilikuwa imeonesha uwezo mkubwa kwa kugeuza matokeo dhidi ya Misri na England katika hatua za mtoano, lakini haikuweza kufanya hivyo tena dhidi ya Hispania.
Kwa ushindi huo, Hispania ilitwaa Kombe la Dunia la wanaume kwa mara ya pili katika historia yake. Aidha, ushindi huo uliifanya Hispania kuwa taifa la kwanza kabisa katika historia kushikilia ubingwa wa Kombe la Dunia la wanaume na wanawake kwa wakati mmoja.
No comments:
Post a Comment