NEWS

Monday, 20 July 2026

Uhusiano wa Tanzania, Misri wapata msukumo mpya



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa na mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Abdel Fattah El-Sisi, Ikulu jijini Dar es Salaam juzi.

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
-------------------

Uhusiano wa Tanzania na Misri umepata msukumo mpya kufuatia ziara ya siku moja ya Rais Abdel Fattah El-Sisi wa Misri kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, jijini Dar es Salaam juzi.

Tanzania na Misri zimekuwa na uhusiano wa kindugu kwa miaka 62 tangu Rais wa Misri huru, Gamal Abdel Nasser, alipoitembelea Tanzania miaka mitatu baada ya uhuru, wakati huo ikiongozwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Kwa miongo zaidi ya sita, nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana katika nyanja mbalimbali muhimu kwa uchumi wa taifa na manufaa ya wananchi wa mataifa hayo.

Rais Samia alisema baada ya mazungumzo na mgeni wake kwamba "tumekubaliana kuimarisha uhusiano katika sekta za kimkakati za biashara na uwekezaji, kilimo, uchukuzi, afya, elimu na nishati."

Alisema nchi hizi mbili zimesaini hati mbili za makubaliano ya ushirikiano na zitazindua Jukwaa la Biashara kuchochea fursa na ustawi wa pamoja.

Aliwataka mawaziri na wataalamu kusimamia kwa karibu makubaliano yaliyofikiwa na nchi hizo ili yawe na manufaa kwa Tanzania.

Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages