NEWS

Tuesday, 7 July 2026

Lori laparamia mnara wa CCM, lapinduka, watu kadhaa wajeruhiwa mjini Tarime




Na Godfrey Marwa
Tarime
--------------

Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa katika ajali ya lori aina ya SHACMAN lenye namba za usajili T 378 EHS lililogonga hadi kuvunja mnara wa CCM kisha kupinduka mjini Tarime, mkoani Mara.

Ajali hiyo ilitokea jana jioni kutokana na kinachoelezwa kwamba ni baada ya lori hilo lililokuwa limepakia kokoto kukata breki kuanzia eneo la Rebu katika barabara ya Nyamwaga.

Baada ya kugonga hadi kuvunja mnara wa CCM katika njia panda ya Tarime-Sirari na Tarime-Nyamwaga, lori hilo liliparamia magari madogo kadhaa kabla ya kupinduka katikati ya barabara.

Taarifa kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa watu waliojeruhiwa akiwemo dereva wa lori hilo walipelekwa kupata huduma za matibabu katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime Rorya hakupatikana haraka ili kuzungumzia ajali hiyo ambayo pia ilisababisha eneo hilo kutopitika kwa magari kwa saa kadhaa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages