NEWS

Monday, 27 July 2026

Mkoa wa Mara una fursa nyingi kwa uwekezaji - RC



Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi.

Na Mwandishi Wetu
Musoma
--------------

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amesema mkoa huo una fursa nyingi za uwekezaji ambazo bado hazijapata uwekezaji wa uhakika katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, madini na utalii.

Kanali Mtambi aliyasema hayo mjini Musoma wiki iliyopita, wakati akizungumza na viongozi wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Meneja Mwandamizi wa Biashara za Serikali za Mitaa, Faraja Kaziulaya.

Aliipongeza benki hiyo kwa kutoa huduma za kifedha zinazochochea maendeleo ya wananchi na ushirikiano na serikali katika ngazi mbalimbali.

Aidha, aliitaka CRDB kuendelea kutoa mikopo kwa wingi kwa wawekezaji wakubwa na wajasiriamali wadogo ili kurahisisha upatikanaji wa mitaji kwa wananchi wenye mawazo mazuri ya biashara wanaotaka kuwekeza katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

“Mkoa wa Mara una fursa nyingi za uwekezaji ambazo bado hazijapata uwekezaji wa uhakika katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, na madini na utalii, hivyo mkiweza kutoa mikopo kwa wingi wananchi watawekeza zaidi,” alisema Kanali Mtambi.

Kwa upande wake Meneja Kaziulaya alisema benki hiyo inaendelea kutoa mikopo kwa wananchi wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi na imerahisisha upatikanaji wa huduma ya mikopo kwa mwekezaji anayetaka kuwekeza nje ya eneo analohudumiwa.

Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages