
Na Mwandishi Wetu
Musoma
-------------
Musoma
-------------
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi (pichani katikati), amewapokea na kufanya mazungumzo na maafisa wa serikali kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo, Wizara ya Afya na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI).
Mapokezi na mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara mjini Musoma jana Alhamisi.
Maafisa hao wanafanya maandalizi ya kampeni ya chanjo ya polio kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 itakayotolewa kuanzia Agosti 27 hadi 30, 2026 katika halmashauri zote za mkoa huo.
Hivyo, wazazi, walezi na wana-Mara kwa ujumla wanahimizwa kuwapa wataalamu wa afya ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi na kuhakikisha kila mtoto aliye katika kundi lengwa anapata chanjo hiyo muhimu.
No comments:
Post a Comment