
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha mgeni wake, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi, Agosti 6, 2026.
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam-------------------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Museveni, leo Alhamisi, Agosti 6, 2026, wameshuhudia nchi hizo kwa kushirikiana na Kampuni ya Vitol ya Ufalme wa Bahrain, zikisaini Hati ya Makubaliano ya Mapendekezo ya Kuendeleza Jiji la Tanga kuwa Kituo cha Nishati cha Kikanda.


“Ninamshukuru Mheshimiwa Rais Museveni kwa ushirikiano unaoendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Uganda na kuleta manufaa kwa wananchi wa nchi zetu.
“Mradi huu ni sehemu ya dhamira yetu ya kuongeza thamani rasilimali zetu na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.
“Utekelezaji wake utapanua fursa za ajira na uwekezaji, kuwezesha wananchi kunufaika zaidi na mnyororo wa thamani wa sekta ya nishati, na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania na Uganda,” Rais Samia ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

No comments:
Post a Comment