Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa Kitengo cha Mawasiliano TANAPA, Catherine Mbena |
Na Mwandishi Wetu
Watu watano, wakiwemo watalii wanne kutoka Uswisi na Mtanzania, wamenusurika kifo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutumbukia mtoni katika eneo la Kogatende ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Eneo la Kogatende ni kivuko cha nyumbu namba moja katika hifadhi hiyo maarufu duniani.
Taarifa iliyotolewa leo na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi - Kitengo cha Mawasiliano cha Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Catherine Mbena, imesema ajali hiyo ilitokea jana Jumapili Agosti 30, 2026 ikihusisha gari lenye namba za usajili T 377 BJE, mali ya kampuni ya utalii ya Nature Responsible Safari.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa gari hilo lilikuwa linaendeshwa na Ramadhani Miraji Mbaga.
TANAPA imewataka madereva, wageni na kampuni za utalii kuzingatia sheria na taratibu za matumizi ya vivuko na kuchukua hatua zote muhimu.
"Uzembe na ukiukwaji wa taratibu unaweza kusababisha madhara makubwa yanayoweza kuepukika kwa kufuata taratibu za hifadhi," imesema sehemu ya taarifa hiyo

No comments:
Post a Comment