NEWS

Sunday, 27 September 2026

CCM yateua Kaimu Makatibu 32 wa mikoa yake, yawaandalia semina elekezi



Kenani Kihongosi

Na Christopher Gamaina

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ya kiutendaji katika safu ya uongozi wake ngazi ya mikoa kwa kuteua Kaimu Makatibu 32 wa mikoa yake yote ya kichama nchini.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Septemba 27, 2026 na kusainiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, imesema viongozi hao wanaanza majukumu yao mara moja.

Sambamba na uteuzi huo, CCM imepanga kuwaandaa viongozi hao kupitia semina elekezi ya siku mbili, itakayofanyika jijini Dodoma kuanzia Septemba 29 hadi 30, 2026.

Semina hiyo imeitishwa na Katibu Mkuu wa CCM, Asha-Rose Migiro, ambapo Kaimu Makatibu hao watapewa mwelekeo wa kiutendaji ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia taratibu, miongozo na vipaumbele vya chama.

Asha-Rose Migiro

Aidha, katika taarifa hiyo, CCM imewapongeza na kuwashukuru Makatibu wa Mikoa waliomaliza muda wao kwa utumishi na mchango wao ndani ya chama hicho tawala.

“Chama kitaendelea kutumia uzoefu na uwezo wa viongozi hao [waliomaliza muda wao] kama sehemu ya hazina ya viongozi na watendaji wake,” imeeleza taarifa hiyo.

Kaimu Makatibu wa mikoa walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Pilly John Jackson (Arusha), Stanley Wilson Mkandawire (Dar es Salaam), Pili Augustine Mbanga (Dodoma) na Ramadhani Kapeto (Geita).

James Dan Mgego (Iringa), Rukia Said Mkindu (Kagera), Salum Khamis Haji (Kaskaz Pemba), Haji Machano Juma (Kaskaz Unguja), Hawa Siri Makonyola (Katavi), Halid Said Mwinyi (Kigoma) na Julius Nansongelya Peter (Kilimanjaro).

Bilal Hussein Maulid (Kusini Pemba), Himid Lussan Tweve (Kusini Unguja), Zuwena Suleiman Mohamed (Lindi), Alawi Haidar Foum (Mkoa wa Magharibi), Yusuph Mabena (Mkoa wa Mjini), Eva Michael Degeleki (Manyara) na Godfrey R. Kavenga (Mara).

Ramadhani Samwel Mahanyu (Mbeya), Joseph Robert Mwega (Morogoro), Ahmada Shaha Vuai (Mtwara), Mwanamasudi Msafiri Pazi (Mwanza), Waridi Josephat Mgumi (Njombe), Abdul-Rahim Hamad “Dodo” (Pwani) na Rehema Nzunye Ndele (Rukwa).

Mohammed Ali Khalfan (Ruvuma), Sophia Abdallah Kibaba (Shinyanga), Kajoro Peter Vyohoroka (Simiyu), Jonathan Mabihya (Singida), Aziza Juma Isimbula (Songwe), Salum Suleiman Tate (Tabora na Twalib K. Berege (Tanga).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages