
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Masanja Kungu Kadogosa kuwa Waziri wa Ujenzi, kuchukua nafasi ya Abdallah Hamis Ulega ambaye ameteuliwa kuwa Wizara ya Katiba na Sheria.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia pia amemteua Dkt. Juma Zuberi Homera kuwa Waziri wa Nishati, ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Wengine ni Asha Khamis Abdalla aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, huku Prof. Bruno Fokas Sunguya akiteuliwa kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Jabiri Omari Makame ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), na Dkt. Idrissa Muslim Hijja ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya UNESCO Tanzania.
“Uapisho wa Mawaziri na Naibu Katibu Mkuu wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye,” ilielezea taarifa hiyo ambayo ilisainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu.
No comments:
Post a Comment