NEWS

Tuesday, 13 October 2026

Kampuni ya Nyambari Nyangwine yazindua vitabu vya utalii kwenye kongamano la kimataifa la biashara



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo (katikati waliokaa), Mwenyekiti wa NNGCL, Nyambari Nyangwine (kushoto waliokaa) na mke wake, Magreth Nyambari (nyuma ya Waziri Akwilapo, mtoto wao, Benson Nyambari Nyangwine (wa tatu kushoto waliosimama), miongoni mwa wengine wakati wa uzinduzi wa vitabu vya kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa uliofanyika jijini Dar es Salaam, Oktoba 11, 2026.

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
--------------------

Vitabu vitatu kuhusu sekta muhimu ya utalii nchini Tanzania vilizinduliwa Ijumaa, Oktoba 11, 2026 jijini Dar es Salaam kwenye Kongamano la Kimataifa la Biashara na Uwekezaji, lililoandaliwa na Nyambari Nyangwine Group of Companies Limited (NNGCL).

Vitabu hivyo, vilivyoandikwa kwa lugha za Kiswahili, Kiingereza na Kifaransa, na Benson Nyambari Nyangwine, vinaelezea uzoefu wa mwandishi huyo baada ya kutembelea maeneo mbalimbali duniani na kujionea vivutio kadhaa ambavyo ni chachu katika kukuza utalii nchini.

Benson ni mtoto wa mwandishi mashuhuri wa vitabu, mfanyabiashara na mwanasiasa Nyambari Nyangwine, ambaye juhudi zake zimezaa matunda ya kuandaa kongamano la kwanza la kimataifa la biashara na uwekezaji nchini.

Mtoto Benson akimlisha keki baba yake, Nyambari Nyangwine, katika kongamano hilo.

Vitabu hivyo vilizinduliwa rasmi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo, kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratias Ndejembi.

Waziri Akwilapo akihutubia kongamano hilo

Kwa mujibu wa mwakilishi wa familia ya Nyangwine, vitabu hivyo sasa vitawekwa kwenye malango mbalimbali nchini, ikiwemo viwanja vya ndege, bandari na mipakani, ikiwa ni jitihada za makusudi kukuza sekta ya utalii.

Mwakilishi huyo alisema jitihada zinafanyika kutafsiri vitabu hivyo kwa lugha nyingine zaidi ya Kiswahili, Kiingereza na Kifaransa.

Mwenyekiti wa NNGCL, Nyambari Nyangwine, akizungumza katika kongamano hilo

Kwa sasa, Serikali ya Tanzania inaweka mkazo mkubwa katika kukuza sekta ya utalii ili iweze kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa taifa.

Uandishi wa vitabu na matangazo ni sehemu muhimu ya kuitangazia dunia vivutio lukuki vya utalii vinavyopatikana Tanzania, ambavyo haviko maeneo mengine katika sayari hii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages