NEWS

Friday, 9 October 2026

Watu 32 wafariki dunia, 37 wajeruhiwa ajali mbili za magari Morogoro




Na Mwandishi Wetu
Morogoro
----------------

Watu 32 wameripotiwa kufariki dunia na wengine 37 kujeruhiwa katika ajali mbili za magari zilizotokea usiku wa kuamkia Oktoba 9, 2026 katika maeneo ya Mkambarani na Mvomero, mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, vifo 28 vimetokana na ajali ya basi la Dream Line T 672 ELT lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mbeya ambalo lililogongana uso kwa uso na lori T 902 ENG katika eneo la Mkambarani.

Basi hilo liliteketea kwa moto, hali iliyofanya shughuli za uokoaji kuwa gumu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kujaribu kuyapita magari yaliyokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari katika eneo lisiloruhusiwa.

Taarifa imeeleza kuwa kati ya miili ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo, 11 bado haijatambuliwa jinsia.

Ajali nyingine iliyothibitishwa na Polisi ilitokea eneo la Miti Bora, kati ya Dakawa na Dumila wilayani Mvomero, ambapo gari la Polisi lililokuwa na askari waliokuwa kazini liligongana na lori aina ya Scania mali ya Kampuni ya ATT.

Kamanda Kantimbo amesema watu wanne walifariki katika ajali hiyo na majeruhi kupelekwa hospitalini.

Wakati uchunguzi ukiendelea, mamlaka husika zinatarajiwa kutoa taarifa itakayobainisha idadi kamili ya watu waliofariki dunia katika ajali ya Mkambarani na utambulisho wao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages