NEWS

Tuesday, 17 November 2026

Watu wawili wafariki dunia kwa kufukiwa na mwamba wakitafuta dhahabu shimoni Nyamongo



Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi (RPC) Tarime-Rorya, SACP Mark Njera.

Na Mwandishi Wetu
Tarime
-------------

Watu wawili wamefariki dunia baada ya kufukiwa na mwamba ndani ya shimo linalomilikiwa na mchimbaji mdogo wa dhahabu katika kijiji cha Mjini Kati kilichopo Nyamongo, wilaya ya Tarime, mkoani Mara.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Mko wa Kipolisi (RPC) Tarime-Rorya, SACP Mark Njera, ajali hiyo ilitokea Novemba 13, 2026 katika kitongoji cha Nyabikondo.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana Jumanne, RPC Njera aliwataja waliopoteza maisha katika tukio hilo kuwa ni Baraka Mwita (20) na Ghati Sati maarufu kwa jina Ghati Pita (28), wakazi wa kijiji cha Muriba, wilayani Tarime.

“Chanzo cha tukio hilo kinadaiwa kuwa ni uzembe wa mmliki wa shimo hilo kutofuata kanuni na taratibu za usalama katika maeneo ya uchimbaji,” alisema.

Hata hivyo, Kamanda huyo alisema uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo unaendelea.

Aidha, RPC Njera alitoa wito kwa wachimbaji wadogo wa madini kufuata kanuni na taratibu za kiusalama katika mazingira yao ya kazi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages