
Lori likiwa kazini katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara
Tarime
--------------
Uvamizi unaofanywa na makundi ya vijana almaarufu kama ‘intruders’, unatishia uzalishaji katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, jambo ambalo pia linaweza kuathri utekelezaji wa miradi ya kijamii, Meneja Mkuu wa mgodi huo, Stephen Dyole amesema.
Hali hiyo inaweza kukwamisha upatikanaji wa mabilioni ya fedha za mpango wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) yanayotolewa na mgodi huo kugharimia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kijamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
Kwa mujibu wa Dyole, vitendo hivyo vimeanza kujitokeza tena katika mgodi huo ambao unaendeshwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals.
Doyle alisema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Mahusiano iliyofanyika Nyamongo juzi, ikiwa ni sehemu ya juhudi zinazofanywa na mgodi huo kuendeleza na kuimarisha uhusiano na vijiji 11 vinavyozungunka.
Aliomba wananchi wa vijiji hivyo na jamii kusaidia kuzuia na kukomesaha vitendo vya uhalifu ambavyo vinatishia uzalishi wa dhahabu katika mgodi huo.
Alitaja baadhi ya vitendo hivyo kuwa ni uvamizi unaofanywa na baadhi ya watu, hususan vijana wanaojulikana kama ‘intruders’, ambao wanaharibu miundombinu na kuingia ndani ya mgodi.

Meneja Mkuu wa mgodi huo, Stephen Doyle, akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo.
Hata hivyo, Dyole alisema mgodi huo utaendelea kuwekeza kwenye maendeleo endelevu katika vijiji hivyo kupitia mpango wake wa CSR.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, naye alitoa wito kwa jamii, viongozi wa vijiji, kata na wazee wa mila kuendelea kudumisha mahusiano mazuri na mgodi huo, akisema ni muhimu kwa uwekezaji na maendeleo endelevu katika eneo hilo.
“Tukivamia mgodi tunarudisha nyuma uzalishaji. Maeneo yaliyo jirani na mgodi huu yamepiga hatua kubwa ya maendeleo. Tutumie vizuri mibaraka hii,” alisema Meja Gowele ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele, akizungumza.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii (CDC) katika Mgodi wa North Mara, Rashid Bogomba, alisema wiki hiyo ya mahusiano itahusisha pia mikutano ya kuzungumza na wananchi wa vijiji 11 vilivyo jirani kuhusu umuhimu wa kudumisha mahusiano mema na kampuni ya Barrick.
“Tutaenda kila kijiji kuzungumza na wananchi ili tuendelee kuimarisha mahusiano yetu na mgodi - wapate kinachostahili, nasi tupate tunachostahili,” alisema Bogomba mabaye pia ni Diwani wa Kata ya Kemambo.

Mwenyekiti wa CDC, Rashid Bogomba, akisisitiza jambo.
Bogomba pia alisisitiza umuhumu wa jamii kushirikiana kukemea vitendo vya wavamizi katika mgodi huo.
“Tutafute namna ya kumaliza tatizo la ‘intrusions’ ili tuendelee kunufaika na fedha za CSR zinazotolewa na mgodi,” alisema Bogomba.
Mgodi huo umekuwa ukitenga wastani wa shilingi bilioni nne kila mwaka kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya jamii kupitia mpango wa CSR.
Taarifa zilizopo zinaonesha kuwa mgodi huo umewekeza shilingi zaidi ya bilioni 30 kutekeleza miradi zaidi ya 250 ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kupitia mpango wake wa CSR tangu 2019 ulipokabidhiwa kwa kampuni ya Barrick hadi sasa.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Stephen Doyle (aliyevaa bukta), Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Meja Edward Gowele (aliyevaa kofia nyekundu) na washiriki wengine wakiwa kwenye mbio fupi wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Mahusiano katika mji wa Nyamongo juzi.
Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara
No comments:
Post a Comment