NEWS

Monday 22 July 2019

SIMBACHAWENE , BASHE WAAPISHWA

 Na mwandishi wetu

Rais John Magufuli ameawapisha viongozi walioteuliwa jana  baada ya kufanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri.

Walioapishwa leo  saa tatu asubuhi ni Waziri mpya wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira), George  Simbachawene  na Naibu Waziri mpya wa Kilimo Hussein Bashe.


Simbachawene amechukua nafasi ya January Makamba ambaye  uteuzi wake ulitengulia na Rais Magufuli jana huku Bashe akichukua  nafasi ya Innocent Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara hivi karibuni.

Rais Magufuli amewataka kutekeleza  majukumu yao vizuri ili kukidhi matarajio ya watazania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages