NEWS

Thursday 14 May 2020

Magendo mpaka wa Sirari yaundiwa kikosi kazi


MKUU wa Wilaya ya Tarime, Mhandishi Mtemi Msafiri, ameunda kikosi kazi kwa ajili ya kupambana na vitendo vya magendo katika maeneo ya mpaka wa Sirari unaotenganisha Tanzania upande wa wilaya ya Tarime na nchi ya Kenya.

Mhandisi Msafiri amechukua hatua hiyo Mei 13, 2020 baada ya kukamatwa kwa bidhaa mbalimbali zikiwa zimefichwa katika stoo bubu zenye thamani ya Sh milioni 14.6, ambapo kodi ya serikali iliyokwepwa kwenye bidhaa hizo ni Sh milioni 17.

Bidhaa zilizokamatwa ni pamojana na mafuta ya kula, chumvi, sukari, tambi, miongoni mwa nyingine.

Kaimu Meneja wa Forodha Mkoa wa Mara, Allan Maduhu, amesisitiza wafanyabiashara kuendelea kufuata taratibu ili serikali iweze kukusanya mapato kwa ajili ya kugharimia utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.

(Habari na  Frankius Cleophace, Sirari)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages