NEWS

Wednesday 13 May 2020

Tarura yarejesha madaraja yaliyoharibiwa Simiyu

WAKALA wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura) Mkoa wa Simiyu imeanza ukarabati wa madaraja mawili yaliyoharibiwa na mvua wilayani Bariadi.

Madaraja hayo ni Ndoba linalotenganisha vijiji vya Bunamhala na Majahida katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Nyambuli linalotenganisha vijiji vya Mwamondi na Lulai katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.

Mratibu wa Tarura Simiyu, Mhandisi Philemon Msomba, ameiambia Mara Online News jana Mei 13, 2020 kwamba ukarabati wa madaraja hayo utagharimu Sh milioni 58.

(Habari na Anita Balingilaki, Bariadi)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages