MKUU
wa Wilaya ya Tarime, Mhandishi Mtemi Msafiri, ameunda kikosi kazi kwa ajili ya
kupambana na vitendo vya magendo katika maeneo ya mpaka wa Sirari unaotenganisha
Tanzania upande wa wilaya ya Tarime na nchi ya Kenya.
Mhandisi
Msafiri amechukua hatua hiyo Mei 13, 2020 baada ya kukamatwa kwa bidhaa
mbalimbali zikiwa zimefichwa katika stoo bubu zenye thamani ya Sh milioni 14.6,
ambapo kodi ya serikali iliyokwepwa kwenye bidhaa hizo ni Sh milioni 17.
Bidhaa
zilizokamatwa ni pamojana na mafuta ya kula, chumvi, sukari, tambi, miongoni
mwa nyingine.
Kaimu
Meneja wa Forodha Mkoa wa Mara, Allan Maduhu, amesisitiza wafanyabiashara kuendelea
kufuata taratibu ili serikali iweze kukusanya mapato kwa ajili ya kugharimia utekelezaji
wa miradi ya Maendeleo.
(Habari
na Frankius Cleophace, Sirari)
No comments:
Post a Comment