SHULE
ya Msingi Murunyigo iliyopo kijiji cha Kiemba, kata ya Ifulifu, jimbo la Musoma
Vijijini, imeboreshewa miundombinu kutokana na michango mbalimbali ya wananchi,
mbunge, serikali na wadau wa maendeleo.
Wadau
wa maendeleo walioshirikiana na Mbunge wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo, serikali
na wanakijiji katika kuboresha miundombinu ya shule hiyo iliyoanza mwaka 1956
ni Shirika la PCI na Benki ya CRDB.
Msaidizi
wa Mbunge, Fedson Masawa, ameiambia Mara Online News leo Mei 4, 2020 kwamba
Benki ya CRDB imechangia vifaa mbalimbali vya kukamilisha ujenzi wa chumba cha
darasa katika shule hiyo.
Afisa
Mtendaji wa Kijiji cha Kiemba, Regina Chirambo, ametaja vifaa vilivyotolewa na
benki hiyo kuwa ni saruji mifuko 60, rangi ndoo mbili na kopo moja, square pipe
tano, flat bar 10, komeo na bawaba.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Kijiji, Rocket Rukiko, amesema Shirika la PCI limejenga vyoo na
kutoa chakula na vitabu kwa wanafunzi na elimu ya afya katika shule hiyo ya
Murunyigo.
Wakazi wa kijiji ch Kiemba wakishiriki katika uboreshaji wa miundombinu ya Shule ya Msingi Murunyigo. |
Kwa
upande wake, Mbunge Profesa Muhongo, amechangia uboreshaji wa miundombinu ya
shule hiyo kwa kutoka saruji mifuko 60, madawati 106 na vitabu mbalimbali kwa
ajili ya maktaba ya shule hiyo.
Mbunge
huyo amesema serikali kupitia mradi wake wa Equit inaendelea kushirikiana na
wananchi katika kuboresha zaidi mazingira ya elimu shuleni hapo.
Profesa
Muhongo, viongozi na wanakijiji wamewashukuru wadau wa maendeleo waliochangia
uboreshaji wa miundombinu ya shule hiyo na kutoa mwito kwa wengine kujitokeza
kuwaunga mkono katika juhudi hizo.
(Habari na
Christopher Gamaina,)
No comments:
Post a Comment